Jeshi la Polisi laonya wanaohamasisha kufanyika vurugu
1 min read

Jeshi la Polisi laonya wanaohamasisha kufanyika vurugu

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini, limewaonya baadhi ya viongozi wa dini, wanaharakati na wanasiasa ambao wamekuwa wakifanya vikao vya siri vya kuhamasiha watu kutaka kujiingiza kwenye uhalifu.

Katika tamko lake kwa umma alilolitoa leo Jumatatu Oktoba 26,2026,  Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime amesema, kumekuwepo na mipango, matamko na uhamasihaji  unaofanywa na viongozi hao kisirisiri kupitia vikao  vya ndani.

Katika vikao hivyo amesema kumekuwepo   na uhamasishaji  wa wazi wenye nia au mwelekeo  wakutaka kuhamasisha watu kutaka kujiingiza kwenye vitendo vya  vya uhalifu.

“Vitendo hivyo vya kihalifu vinavyopangwa ni pamoja na kufanya  vurugu au  fujo,kuharibu miundombinu inayotumiwa  kutoa  huduma kwa  umma, mali za umma  na binafsi.

“Jeshi la Polisi Tanzania  linawahakikishia kwa kushirikiana na vyombo  vingine  vya ulinzi na usalama na kwa kutumia taarifa  zinzoendelea kupokea  linafuatilia  kwa karibu ikiwa ni pamoja na kuwakamata  wahusika  wa mipango hiyo kwa hatua zaidi za kisheria,”ameeleza Misime kwenye taarifa hiyo.

Aidha ametoa onyo kwa wanaojihusisha kwa namna moja au nyigine katika vitendo hivyo vya uhalifu  vyenye mwelekeo wa kufanya fujo na kuharibu mali,  kuacha  kwani jeshi hilo halitasita kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria kwa yotote ataatakayebainika kujihusisha na mipango hiyo ya kihalifu .

Kwa upande wa wananchi, jeshi hilo limetoa wito  kwa kuendelea kuzingatia sheria za nchi na utii wa sheria bila shuruti kwa kuwa ndio msingi wa aman, utulivu na usalama wa Taifa.

“Jeshi la Polisi  Tanzania  linaenedelea kutekeleza majukumu yake ikiwemo kulinda amani, utulivu  na usalama,”amesema Misime .

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *