Kilomita 59 za lami zajengwa Mji wa Serikali Mtumba
1 min read

Kilomita 59 za lami zajengwa Mji wa Serikali Mtumba

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Profesa Riziki Shemdoe amesema barabara za lami zenye urefu wa kilomita 59.1 zimejengwa katika Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma.

Mbali na hizo, Shemdoe kuna kilomita 59.1 zimejengwa kwa ajili ya watembea kwa miguu na kilomita 59.1 kwa waendesha baiskeli.

Amesema hayo leo Ijumaa, Oktoba 30, 2026, mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyeambatana na mwenyeji wake Rais wa Angola, João Lourenço, kabla ya wawili hao kuzindua barabara hizo.

Muonekano wa baadhi ya miundombinu iliyojengwa katika Mji wa Serikali uliyopo Mtumba jijini Dodoma. Picha na Maktaba

“Barabara hizi zipo katika eneo lote la Mji wa Serikali ikiwemo ofisi za balozi ya nchi ya Angola itakapojengwa.Pia barabara zote zimewekwa taa 1635, kwa hiyo mheshimiwa Rais ukipita usiku hapa, hali ni tofauti kabisa,” amesema Shemdoe.

Katika hatua nyingine, Shemdoe amemshukuru Rais Samia kwa kutoa majina ya marais wastaafu katika barabara hizo, ikiwemo ya barabara ya Julius Nyerere,

Muonekano wa baadhi ya miundombinu iliyojengwa katika Mji wa Serikali uliyopo Mtumba jijini Dodoma. Picha na Maktaba

Kwa mujibu wa Profesa Shemdoe, katika kilomita 51. 1, kuna kilomita 11.7 zimejengwa kwa mfumo wa ‘double lane’ na kilomita 36 ni single line.

Aidha, Shemdoe amesema vituo vya mabasi 52 vimejengwa, sambamba na mabwabwa matatu yatakayosaidia kuepusha mafuriko kwa kuzuia maji yasitoke katika Mji wa Serikali.

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *