Habari za Dharura
Your blog category
Wadau washauri Oktoba 29 iwe siku ya kusaka amani
Dar es Salaam. Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeitaka Serikali kutenga Oktoba 29 ya kila mwaka kuwa siku ya kitaifa ya kumbukizi ya waathirika wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Mtandao huo umemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kulifanyia kazi pendekezo hilo, ukisema siku hiyo […]
Wapiga kura wa Netanyahu waanza kumgeuka
Israel. Baadhi ya wafuasi wa muda mrefu wa chama cha Likud cha Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu wameanza kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba kuwahamasisha wapiga kura kumuunga mkono mpinzani wake, Gadi Eisenkot, wakisema Israel inahitaji mabadiliko ya uongozi. Mabadiliko hayo yanajitokeza katika mji wa Dimona, uliopo katika Jangwa la Negev, ambao kwa muda mrefu umekuwa […]
UDSM yaadhimisha miaka 65 kwa elimu, tafiti, uhifadhi mazingira
Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwake, kikijivunia mchango wake katika elimu ya juu, tafiti na kuandaa viongozi, huku kikiweka mbele umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kampasi kuu ya chuo hicho jijini Dar es Salaam, leo Jumapili, Oktoba […]
Same yatenga siku saba kudhibiti tembo
Same. Serikali ya Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, inatarajia kuanza operesheni ya siku saba ya kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu, hususan tembo wanaovamia makazi na mashamba ya wananchi na kusababisha majeraha pamoja na uharibifu wa mazao. Operesheni hiyo inatarajiwa kuanza kesho, Oktoba 26, 2026, kwa ushirikiano kati ya Serikali ya wilaya na taasisi za uhifadhi, […]
Ulevi wa gongo kwa vijana Rombo, Moshi waibua hofu
Kilimanjaro. Unywaji wa pombe kupita kiasi, ikiwamo gongo kwa baadhi ya vijana wilaya za Rombo na Moshi mkoani Kilimanjaro, umeibua hofu kwa wadau, wakisema hali hiyo inaathiri afya, kipato na mustakabali wa familia. Wakizungumza hivi karibuni, baadhi ya viongozi wa dini na wananchi wamesema vijana wanaotumia muda mwingi kunywa pombe wanashindwa kujishughulisha na shughuli za […]
Wabeba mizigo hatarini kupata matatizo ya mgongo, nyonga
Mbeya. Vijana wanaojishughulisha na ubebaji wa mizigo mizito kwa kutumia mgongo, mabega na kichwa maarufu ‘makuli’ wako hatarini kupata matatizo ya mifupa na viungo, ikiwamo pingili za mgongo. Wakati wataalamu wa afya wakisema hivyo, makuli wenyewe wanasema baadhi yao hawana elimu kuhusu hatari tarajiwa ya kazi zao na hata wanapohisi maumivu ya mgongo wengi hukimbilia […]
Chadema yadai kushambuliwa na Polisi, Msajili
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai kuwa kinapitia mashambulizi kutoka Jeshi la Polisi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ili kipoteze mwelekeo wa ajenda ya kuwatetea maslahi ya Watanzania. Kwa mujibu wa Chadema, mashambulizi hayo yanajumuisha kukamatwa na kuachiwa kwa baadhi ya viongozi wake kwa nyakati tofauti, pamoja na […]
Migogoro 21 ya ndoa yaripotiwa ndani ya siku 23 Mwanza
Mwanza. Jumla ya migogoro 21 ya ndoa imeripotiwa katika vituo vya polisi mkoani Mwanza kuanzia Oktoba Mosi hadi 23, mwaka huu, huku wivu wa mapenzi, usaliti na changamoto za kiuchumi zikitajwa miongoni mwa sababu zinazochangia migogoro hiyo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amesema wivu wa mapenzi umekuwa ukitajwa mara kwa mara katika […]
Teknolojia ya kupima viinitete yazindua ukurasa mpya wa huduma za uzazi
Dar es Salaam. Wanandoa wanaokabiliwa na changamoto za kupata watoto, kuharibikiwa na mimba mara kwa mara au hatari ya kurithisha watoto magonjwa ya vinasaba sasa wanaweza kunufaika na teknolojia ya uchunguzi wa viinitete kabla ya kupandikizwa kwenye mfuko wa uzazi. Teknolojia hiyo, inayojulikana kama Preimplantation Genetic Testing (PGT), hutumika kuchunguza baadhi ya hitilafu za kromosomu […]
Fanya haya kuepuka wizi wa fedha mtandaoni
Dar es Salaam. Matumizi ya namba moja ya siri katika akaunti mbalimbali za huduma za kifedha na kutumia mwaka wa kuzaliwa kama namba ya siri ni miongoni mwa mianya hatari inayoweza kutumiwa na matapeli wa mtandaoni kuiba fedha zako. Hatari hiyo hujitokeza pale wahalifu wanapofanikiwa kupata namba ya siri ya huduma moja na kuijaribu katika […]